Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali
imewataka wananchi kushiriki kikamilifu uanzishwaji wa viwanda vidogo
vya kusindika vitunguu Saumu na Mazao mengine ya Biashara katika maeneo
yote hapa nchini.
Akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Martha Umbulla, Waziri wa Viwanda
Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa mazao ya Pareto
na Vitunguu saumu yanayolimwa katika Wilaya ya Mbulu na maeneo mengine
yana thamani kubwa na yanaweza kuchochea na kuhamasisha uanzishwaji wa
viwanda vya kusindika mazao hayo.
“
Kwa kutambua faida zitokanazo na zao la pareto, Serikali iliamua
kuanzisha Bodi ya Pareto kwa lengo la kudhibiti uzalishaji, usindikaji
wa biashara ya pareto hapa nchini” Alisisitiza Mhe. Mwijage
Akifafanua
amesema kuwa Serikali itaendeleza juhudi za kuhamasisha uwekezaji
kwenye viwanda vya kuengua na kuchuja pareto ili kuongeza thamani ya zao
hili na kuwanufaisha wananchi katika maeneo yanayolima pareto ikiwemo
Wilaya ya Mbulu.
Kwa
upande wa zao la Vitunguu saumu Wizara ya Viwanda kupitia karakana za
SIDO katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro zinatengeneza “Blender”
ambayo itatumika kusaga zao hili kuwa katika mfumo laini ‘’ Garlic
Paste” teknolojia hiyo inapatikana kwa gharama ya shilingi milioni moja
na laki nane.
Aidha,
SIDO imekuwa ikitoa mafunzo kwa vikundi na watu binafsi juu ya
usindikaji wa zao la vitunguu saumu katika mikoa inayolima zao hilo.
Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa
ikihamasisha na imefanikiwa katika kuvutia wawekezaji na wananchi
kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment