Jeshi
la Magereza limesema mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi
maarufu Sugu ametoka kwa msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa kwa
wafungwa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, Aprili 26, 2018.
Ofisa
habari wa jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje amesema
katika maadhimisho hayo, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa
3,319, kati yao wafungwa 585 waliachiliwa huru Aprili 26, 2018.
“Wafungwa
2,734 walibakia gerezani akiwemo Sugu kumalizia sehemu ya kifungo
kilichobakia baada ya kupewa msamaha huo na Rais Magufuli,” amesema.
0 comments:
Post a Comment