Mbunge
wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ameachiwa huru
leo Mei 10, 2018 kutoka katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya alikokuwa
amefungwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga,
amefunguka na kuweka wazi kilichojiri.
Amesema
hakuwa anafahamu iwapo angeachiwa huru leo hadi polisi walipomfuata na
kumwambia ajiandae. Amedai mapaka sasa hafahamu imekuwaje hadi akaachiwa
kwani ilijulikana ataachiwa Juni 5, ambapo kifungo chake kingekamilika.
“Watu
wote walitarajia ningetoka jela mwezi Juni, lakini ghafla jana
niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi (leo) natakiwa niachiwe huru,
nilipotoka nje nikakuta askari wengi, nikaelekezwa kuingia kwenye gari
la RCO mimi na mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maofisa magereza
watano hadi nyumbani na kutukabidhi kwa familia.
“Watu
wanauliza, imekuwaje? Lakini mimi ninawaambia sijui, kwa sababu haikuwa
kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa
sababu mimi ninachoamini sikutakiwa kuwa magereza in the first place,
utumishi uko palepale kwa level ileile, tulikuwa na exposure sasa hivi
tumeongeza experience,” amesema Sugu.
Sugu
na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela
Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa
lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara
walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini
Mbeya.
Wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.
0 comments:
Post a Comment