Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).
Taarifa
hiyo imetolewa leo asubuhi Mei 11, 2018 bungeni mjini Dodoma na
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na kubainisha kuwa mbunge huyo kijana
amechaguliwa jana kwa kishindo.
“Umelipa
Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla. Nafasi hii ni ya kuitangaza
nchi yetu na Bunge hili tunamtakia kazi njema,” amesema Chenge ambaye
pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM).
“Nampongeza
sana kijana huyu, lakini pia Serikali kwani huwezi kupata nafasi hii
kubwa kama huungwi mkono na Serikali. Nimpongeze sana Rais John
Magufuli.”
0 comments:
Post a Comment