Hospitali
ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila imezindua rasmi kitengo cha huduma ya
uchujaji damu (dialysis) kwa wagonjwa wa figo.
Kitengo
hicho kimezinduliwa jana Mei 8 na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya na wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Dk. Ulisubisya alisema kitengo hicho kimewekwa
jumla ya mashine 12 na kwamba kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya
wagonjwa 10,000 kwa mwaka wakiwamo wasio na maambukizi na wenye
maambukizi.
“Kitengo
hiki kinachoongozwa na madaktari bingwa wazoefu na wauguzi wenye ari,
kitakuwa kituo-darasa cha tiba makini kwa wagonjwa wote, vile vile kituo
hiki kitatoa mafunzo endelevu kwa madaktari wajao na kitakuwa chachu ya
tafiti zenye kutoa miongozo ya matibabu na kuboresha sera za matibabu
ya wagonjwa ya figo nchini,” alisema.
Naye,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard
Akwilapo amesema kwa kipindi cha miezi sita hadi sasa tangu kuzinduliwa
kwa MAMC tayari jumla ya wanafunzi 350 wamepokea mafunzo mbalimbali ya
udaktari na udaktari bingwa.
0 comments:
Post a Comment