Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka
mitatu mkazi wa kijiji cha Keringet kaunti ya Pokot amekutwa na sindano 7
za kushonea kwa mkono tumboni mwake, baada ya kupigwa picha ya xray.
Mtoto huyo alipelekwa hospitali ya
Kapenguria siku ya Jumanne kupata matibabu ya maumivu ya tumbo ambayo
alikuwa akiyapata kwa muda mrefu bila kujua tatizo ni nini.
Bibi yake Bi. Emily Linga'a ambaye ndiye
anayeishi naye, amesema mtoto huyo alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo
kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawakuweza kubaini mara moja chanzo
cha maumivu hayo na kuendelea kumpatia dawa za kutuliza maumivu, lakini
baada ya kuona anazidi kualalamika walimpeleka hospitali na kugundua ana
tatizo hilo.
“Kwanza nilidhani mtoto alikuwa na
minyoo, sikuwahi kufikiria kwamba ana sindano tumboni mwake, nilikuwa
nahisi ni malaria siku zote na kumpa dawa za maumivu”, amesema bibi huyo
ambaye anaishi naye, baada ya mama yake kumuacha alipoolewa na mwanaume
mwengine.
Madaktari wa hospitali hiyo wamempa
rufaa ya kwenda hospitali kubwa ya Moi ili kuweza kufanyiwa upasuaji wa
tumbo, na kutolewa sindano hizo ambazo hazijajulikana zimeingiaje.
0 comments:
Post a Comment