Muigizaji
wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuelezea mipango yake
aliyonayo kuhusu kipindi chake kinachotarajiwa kurushiana ndani ya
Wasafi Tv.
Kama
utakumbuka siku za nyuma kidogo Wema aliweka wazi kuwa hana Mahusiano
ya kimapenzi na Diamond bali atakuwa na uhusiano wa kikazi naye kwani
atakuwa bosi wake.
Wema alitangaza kuwa atakuwa na kipindi ndani ya Wasafi Tv ambayo imeanza kurusha matangazo yake wiki chache zilizopita.
Wema
amefunguka hayo kwenye press conference aliyofanya kuweka wazi kitakuwa
ni kipindi cha kawaida na sio reality show kama ilivyokuwa mwanzoni
kwenye EATV.
"Kitakuwa
ni kipindi cha tofauti tutakuwa wanadada watatu. Sitapenda kuweka wazi
zaidi lakini haitakuwa reality show, kama itakuwa ni reality show
nitaweka kwenye App yangu.
"Bado
hatujaanza ku-shoot kwa sababu sasa hivi bado wanafanya majaribio, kwa
hiyo ile process nzima ya vipindi bado haijanza, so content zipo pale
pale na tutaanza ku-shoot hivi karibuni”.
0 comments:
Post a Comment