Muigizaji wa filamu Bongo Mwanaheri Afcely kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya tuhuma za kuwa kikojozi.
Mwanaheri amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote na watu walioanzisha hizo habari wana wivu juu ya ndoa yake.
“Hakuna
ukweli wowote, sijawahi kujikojolea hata siku moja, mimi ni msanii huwa
nalala kambini, wapigie simu kina JB waulize kama kuna siku nimewahi
kukojoa, jamani hii ndoa watu imewauma, mpaka kunizushia habari za
uongo!! Sio kweli mimi sio kikojozi, ila nina tatizo la pumu tangu
utotoni”, amesema Mwanaheri.
Taarifa
za mlimbwende huyo aliyejaliwa shepu ya kiafrika kutoka zilitolewa na
mmoja wa watu wake wa karibu, na kusema kwamba msichana huyo ana tatizo
la kujikojolea kitandani alilokuwa nalo tangu utotoni.
0 comments:
Post a Comment