Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amehoji ni kwanini Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Utumishi, George Mkuchika akaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni
wakati kanuni za bunge haziruhusu.
Amesema
kwa mujibu wa kanuni za bunge, mwenye sifa ya kukaimu nafasi hiyo ni
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi ambaye
ndiye ana muda mrefu bungeni.
“Uwepo
wa Mkuchika katika nafasi hiyo umechangiwa na nafasi yake ya udhamini
katika Klabu ya Yanga kwa kuwa viongozi wa Yanga wanapenda sana
madaraka,” amesema.
Kutokana
na hali hiyo, Zitto alitaka Waziri Mkuchika aachie nafasi hiyo kwa kuwa
uwepo wake katika nafasi hiyo anakiuka kanuni za bunge.
Akijibu
hoja hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema Mkuchika
alikaimishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati Dk. Mwinyi akiwa na
shughuli nyingine nje ya bunge.
“Kutokana
na hali hiyo, Mkuchika ataendelea kushika nafasi hiyo hadi Waziri Mkuu
atakapofanya mabadiliko mengine,” amesema Jenista.
0 comments:
Post a Comment