Mbunge
wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini amewaonya viongozi wa kisiasa
kutolitumia Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa shughuli za
siasa.
Selasini
ameshauri JWTZ kutumia kitengo chake cha upelelezi kulisaidia Jeshi la
Polisi ambalo amedai limeshindwa kubaini matukio ya ajabu yanayoiaibisha
nchi.
Hayo
ameyasema leo Mei 14, 2018 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia
Bajeti ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 2017/18 huku
akiwapongeza Waziri wa Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa
Majeshi, Venance Mabeyo kwa uongozi mzuri.
“Mimi
nishauri tu, jeshi letu linaheshima katika majeshi ya Afrika, heshima
yake inatokana na misingi yake na hili ni jeshi letu, ninaomba wanasiasa
na viongozi wetu tusilichafue jeshi hili kama tulivyolichafua jeshi la
polisi,” amesema Selasini na kuongeza:
“Leo katika nchi yetu, ikitokea ajali ya polisi, watu wanauliza wamekufa wangapi.”
Selasini
amesema, “Hata katika operesheni ya Ukuta (Umoja wa Kupambana na
Udikteta Tanzania), wanajeshi walionekana wanafanya mazoezi, jeshi
linalinda usalama wa mipaka, kwa nini tunalishughulisha na mambo
yanayofanywa na polisi.”
Kuhusu upelelezi, Selasini amesema Mkuu wa Majeshi namshukuru atumie kitengo chake cha upelelezi.
“Ili
haya matukio ya aibu, iko hofu, watu wanasema kuna maeneo nyeti nchini
sasa yanalindwa na askari kutoka nchi hususan Rwanda, sasa hofu hiyo ya
watu wasiojulikana inatia hofu.”
0 comments:
Post a Comment