Nchi ya Burundi leo inapiga kura ya maoni kufanya marekebisho ya katiba
ambayo yanaweza kumuweka Rais wa sasa Pierre Nkurunziza madarakani mpaka
mwaka 2034
Kwa mujibu wa BBC Kura hiyo itapigwa ya ndiyo au hapana ili kuongeza
muda wa Rais kukaa madarakani kutoka miaka mitano mpaka saba katika
awamu moja.
Katiba ya sasa imeweka ukomo kwa Rais aliyepo madarakani kuhudumu kwa
kipindi cha awamu mbili, kwa mujibu wa mabadiriko yatakayofanywa yatampa
uhuru Rais Nkurunziza kugombea tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
akiwa kama mgombea mpya na hivyo huenda akatawala mpaka mwaka 2034.
Chama tawala CNDD-FDD kinachoongozwa na Nkurunziza ndicho kinaendesha
kampeni ya kuunga mkono upigwaji wa kura ya ndiyo huku kiongozi wa
upinzani Agaton Rwasa chini ya mwamvuli wa muunganiko wa vyama vya
upinzani ujulikanao kama Amizero y’Abarundi wakihamasisha kura ya
hapana.
Thursday, May 17, 2018
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment