Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole Sosopi amesema kwamba hawataki
Mwanasheria wa chama chao, Tundu Lissu akirudi Tanzania awe mtu wa
kuhudhuria kliniki kwa ajili ya matibabu bali wanatarajia aingie kwenye
'struggle' moja kwa moja.
Ole
Sosopi ameyasema hayo jana wakati akijibu swali kwenye Kipindi cha
Kikaangoni kinachorushwa na EATV, na kuongeza kwamba wanatarajia
kiongozi wao atarudi nchini mara tu atakapomaliza matibabu yake
anayoendelea nayo huko nchini Ubelgiji.
"Tundu
Lissu tunataka akirudi asirudi ku-atend clinic, aje aingie kwenye
mapambano moja kwa moja. Lissu ni kama kaka kwangu, alipopigwa risasi
nilifadhaika sana, mpaka kesho nawaza hawa watu walikuwa na dhamira
gani" Ole Sosopi.
Aidha
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa "Lissu ni 'asset' kwa Tanzania na Mungu
amemponya kutuonyesha, na ndio maana yupo mpaka leo".
Lissu
ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa Chadema
alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 alipokuwa kwenye
maeneo ya nyumbani kwake Area D Jijini Dodoma wakati alipokuwa akirejea
kutoka katika majukumu yake.
0 comments:
Post a Comment