Hatua
ya Rais Donald Trump wa Marekani, ya kutangaza kwamba nchi hiyo
inajiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa mpango wa kuizuia Iran
kutengeneza silaha za nuklia, JCPOA, imepokelewa kwa hisia kinzani na
wabunge wa Marekani na viongozi mbalimbali ulimwenguni kote.
Wabunge wengi wa chama cha Demokratik wameikosoa huku Warepublikan wakiisifu kama hatua ifaayo.
Speaker wa bunge, Paul Ryan, ambaye ni Mrepublikan, aliutaja mkataba huo kuwa ulikuwa na hitilafu kubwa.
Lakini
kiongozi wa wachache kwenye bunge hilo, Nancy Pelosi alimshutumu Trump
na kusema kwamba katika uamuzi wake, rais huyo hakutilia maanani ukweli
kwamba mkataba huo ulikuwa unafanya kazi kama ulivyokusudiwa.
Rais
wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kupitia ujumbe wa Twitter aklisema kuwa
nchi yake, Ujerumani na Uingereza "zimesikitishwa mno na hatua hiyo ya
Trump."
Mapema Jumanne, Macron alisema kuwa Ufaransa itaendelea kuunga mkono mikakati ambayo itaimarisha usalama katika eneo hilo.
Katika
hotuba iliyosubiriwa na wengi, RaisTrump alitangaza Jumanne kwamba
ameamua kuiondoa Marekani kutoka mkataba wa kimataifa juu ya mpango wa
kuizuia Iran kutengeneza silaha za nuklia, JCPOA.
Akizungumzia
kutoka Ikulu, Trump alisema ataiwekea tena Iran vikwazo vikali vya
kiuchumi vilivyondolewa wakati wa kufikiwa mkataba huo na mataifa
mengine matano yenye nguvu duniani pamoja na Iran mwaka 2015.
Washirika
wa Ulaya hasa Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, wamekuwa wakijaribu
kumshawishi kiongozi huyo kutochukua hatua hiyo ambayo wanasema ndio
njia pekee ya kusimamia na kufuatilia harakati za nuklia za Iran.
Kabla
ya hatua hiyo ya Trump, Iran ilikuwa imeeleza kwamba haingekubali
kujadiliana tena juu ya mkataba mwengine na Marekani, na kwamba kwa
kujiiondoa, Marekani ingekuwa inakiuka mkataba uliopo na kwamba
itaendelea na mipango yake.
Wizara
ya fedha ya Marekani ilitoa taarifa Jumanne kuwataka Wamarekani wote
walioanza uhusiano na Iran chini na makubaliano hayo, kuanza kusitisha
kazi zao.
0 comments:
Post a Comment