Msanii
Kiwango wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza sababu ya kushindwa
kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu fupi ya dakika 20 ‘MAMA’ ya Aunt
Ezekiel iliyofanyika usiku wa jana (Jumapili) Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
Madam
Sepenga ametoa taarifa hiyo kupitia kwenye mtandao wa Instagram akidai
kuwa alichelewa kutokana na Mama yake ndio alimchelewesha na kujikuta
ameshindwa kufika kwenye uzinduzi huo.
“I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…😩😩😩,” ameandika Wema kwenye mtandao huo.
Hata
hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema
Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni
la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo
kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.
0 comments:
Post a Comment