TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha mahakamani
Ofisa Usafirishaji wa Kampuni ya Athwal Transport & Timber LTD ,
Godfrey Tarimo, kwa mashitaka ya kutoa rushwa kwa mtumishi wa kampuni
hiyo akiri kosa la wizi.
Tarimo alipandishwa kizimbani jana, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Tabora Jackton Rushwela .
Wakili wa Takukuru, Simon Mashingia alidai Tarimo alitenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu katika Gereza la Uyui mjini hapa.
Wakili
Mashingia alidai kuwa siku hiyo mshtakiwa akiwa ni Ofisa Usafirishaji
wa ATT alitoa rushwa ya Sh 400,000 kwa Said Hamis ambaye alikuwa utingo
wa gari katika kampuni ya ATT.
Akifafanua
katika mashitaka hayo, wakili Mashingia alidai kuwa Tarimo akiwa kama
wakala wa kampuni alitoa fedha hizo kama kishawishi kitakacho mfanya
Hamisi akiri kosa la wizi katika kesi ya jinai namba 13/2015 iliyokuwa
inamkabili.
Ilidaiwa
kwamba, Hamisi baada ya kupokea fedha hizo alipofika mahakamani alikiri
kosa ambapo Hakimu Rushwela alimpa adhabu ya kifungo cha miaka mitano
jela. Mwendesha mashitaka alidai, uchunguzi umebaini kuwa Tarimo
alipoteza tumbaku iliyokuwa inasafirishwa na magari ya kampuni ya ATT.
Alidai
kwamba, ili kampuni hiyo isionekane ina sura mbaya katika biashara,
walimbambikia kesi utingo huyo na kumshawishi akubali kuwa ndiye aliiba
ili baadaye waweze kumsaidia atoke lakini alihukumiwa kifungo.
0 comments:
Post a Comment