Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07 Julai, 2016.
Kabla
ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
Dkt.
Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma
Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
08 Julai, 2016