Umoja
wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM
unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la
Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa
mkutano huo.
Akiwa
katika Ofisi za UVCCM – Dodoma jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka
Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika mjini hapo pamoja na
mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho
lakini hawaoni BAVICHA.
“Nipo
hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama
na viongozi wetu, kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa
bahati mbaya kwa muda wote sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii
inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,” alisema Shaka.
Aliongeza
kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya
kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti
wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho
tawala.
Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.
Juzi,
BAVICHA walitangaza kurudi mjini Dododoma kwa lengo la kufanya Mkutano
wao wa Kamati ya Kiutendaji baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman
Mbowe kuwataka kusitisha adhma ya kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa
CCM.