Chama
cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuwaruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu
wafanye siasa vyuoni kwa taratibu zilizowekwa kwa sababu vyuo ni kitovu
cha mabadiliko ya jamii.
Wito
huo umetolewa jana Mei 13 na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
wa chama hicho, Ado Shaibu ambaye anapinga kauli ya Rais John Magufuli
aliyoitoa alipotembelea Chuo cha Kilimo cha Sokoine (Sua) kuwataka
wanafunzi wasifanye siasa vyuoni.
Shaibu
alisema historia inaonyesha kwamba viongozi wengi wa taifa hili
walishawahi kuwa viongozi wa serikali za wanafunzi walipokuwa vyuoni.
Amesisitiza kwamba maisha ya siasa wakiwa vyuoni ndiyo yaliwapa ujasiri
wa kuingia kwenye ulingo wa siasa.
"Kupiga
marufuku siasa vyuoni ni kujenga taifa la vijana waoga, wasiokuwa na
uwezo wa kuhoji. Vijana msiache kuhoji mambo ya msingi kwa jamii zenu,
hiyo ndiyo maana ya usomi," alisema Shaibu.
Katibu
huyo alitoa mifano ya baadhi ya viongozi waliokuwa viongozi vyuoni kuwa
ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba ambaye amesema mwaka
1965 alikuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu hapa
nchini.
Alimtaja
pia Spika wa zamani, Samuel Sitta ambaye pamoja na wenziwe walifukuzwa
chuo mwaka 1966 kwa kufanya mgomo kupinga matabaka hapa nchini, ajenda
ambayo Mwalimu Nyerere aliibeba kwenye Azimio la Arusha.
"Siasa
za vyuo vikuu zimewekewa utarabitu wake, sasa tukianza kuwadhibiti hata
vijana walio vyuoni tunatengeneza taifa la namna gani?" Alihoji Shaibu
na kusisitiza kwamba serikali ina wajibu wa kuhamasisha vijana kujitosa
kwenye siasa ili Taifa lipate viongozi bora siku zijazo.
0 comments:
Post a Comment