Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Nyanda za
Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda
Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya
kukutwa na hatia ya uchochezi.
Wawili
hao wamepokelewa uraiani leo Mei 10, 2018 asubuhi na Mwenyekiti wa
CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama
hicho waliosafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mapokezi hayo.
Sugu
na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela
Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa
lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara
walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini
Mbeya.
Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.
0 comments:
Post a Comment