Dunia inakwenda spidi sana! Miezi kadhaa baada ya staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumwagwa na mama watoto wake, Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’, bado mambo ni moto huku mwanamama huyo
akidaiwa kuzima ngebe au mbwembwe za jamaa huyo, Risasi Mchanganyiko
limedokezwa.
Wakati Diamond akibadili rangi ya lile gari lake aina ya BMW X6 kutoka
nyeusi kwenda bluu bahari, Zari yeye alijibu mapigo kwa kununua gari la
kifahari aina ya Range Rover Spot lenye rangi nyeupe na kuibua gumzo
kubwa kwa mashabiki wao.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, Diamond aliamua kulibadili
gari hilo rangi kwani lilikuwa limezoeleka mitaani jijini Dar tangu
alipopewa kama zawadi siku ya bethidei yake mwaka 2014 alipokuwa
akitimiza umri wa miaka 25. Mbali na kubadili rangi ya gari hiyo, pia
alibadilisha ‘rim’ za matairi yake na kuweka nyingine kali zaidi ya zile
za awali.
Watu walioko karibu na Zari walidokeza kuwa, mfanyabiashara huyo alivuta
ndinga hilo wikiendi iliyopita na kuthibitisha kwamba, yeye ni Boss
Lady wa ukweli ambaye anaweza kufanya makubwa hata bila kuwa na
mwanaume, tofauti na wengi walivyodhani kwamba kummwaga Diamond ndiyo
utakuwa mwisho wake. Vyanzo vilikwenda mbali zaidi na kutaja thamani ya
gari hilo la Zari kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 171 huku lile la
Diamond likiwa na thamani ya shilingi milioni 150.
Zari alitangaza mpango wake wa kununua gari hilo wiki chache zilizopita
na hatimaye wikiendi hii alilianika gari hilo jipya na kuliweka kwenye
mitandao ya kijamii. Zari alitimiza azma yake hiyo kama alivyoahidi
mapema mwaka huu kwamba, kuna mambo alipanga kuyafanya ndani ya Mwaka
2018 ikiwemo kulimiliki gari hilo.
Hata hivyo, mara baada ya kuliweka gari hilo kwenye ukurasa wake wa
Instagram na kuandika; ‘Come through baby girl’, baadhi ya watu walidai
kwamba, gari hilo amenunuliwa na mwanaume wake mpya ambaye ni
mfanyabiashara maarufu jijini Dar (uchunguzi wetu ukikamilika
tutamwanika).
Kufuatia madai hayo, Zari alikanusha kupitia ukurasa wake wa Snapchat
ambapo aliweka wazi kuwa amelinunua kwa fedha zake mwenyewe. Mbali na
gari hilo, mwaka huu, Zari pia aliahidi kuanzisha migahawa mikubwa kama
KFC au McDonalds.
Ili kusikia maoni yake juu ya kufuru za Zari ambazo zimelenga kumkata
ngebe, katika harakati za kumsaka Diamond gazeti hili lilifika kwenye
ofisi mpya za Wasafi zilizopo Kwazena, Mbezi-Beach ambapo lilijuzwa kuwa
jamaa huyo alikuwa nchini Uingereza kikazi.
Alipotafutwa kwa njia ya WhatsApp, Diamond hakujibu ‘chatting’ hivyo
jitihada zinaendelea ili kupata maoni yake. Hata hivyo, mmoja wa watu
waliokutwa ofisini kwake alisema hawezi kuzungumzia masuala binafsi
badala yake aulizwe mambo ya kazi yake ya muziki.
Zari, mbali na gari hilo, pia alishaanika umiliki wake wa magari ya
kifahari kama Mercedez Benz, Audi, Hammer, Ferrari na mengineyo huku
Diamond akimiliki magari mengine kama Toyota Prado, Toyota Land Cruiser
V8 na mengine madogomadogo.
Thursday, May 10, 2018
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment