Mkazi
wa wilayani Igunga, mkoani Tabora ameuawa na fisi na mwingine
kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na mnyama huyo katika Kata ya Ziba,
wakati wakirejea nyumbani kutoka kwenye klabu ya pombe.
Azizi
Kombe, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ziba, alimtaja aliyeuawa ni Mwajuma
Masanja (37), mkazi wa Kijiji cha Iduguta wilayani Nzega na Shija
Maneno (35), mkazi wa Kitongoji cha Ipuli Kijiji cha Igumila Kata ya
Ziba ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufani Nkinga na hali yake ni
mbaya.
Mtendaji
huyo alifafanua watu hao walikuwa ni mtu na mpenzi wake ambao walikuwa
wakinywa pombe za kienyeji kwenye klabu iliyopo Kata ya Ziba na kuongeza
kuwa baada ya kufika saa 3 usiku waliamua kuondoka kurudi nyumbani.
Hata
hivyo, Kombe alibainisha wakati wakiwa njiani kurejea nyumbani
walishambuliwa na fisi eneo la vichaka ambapo alimng’ata Mwajuma sehemu
za makalio na tumboni, hali iliyomlazimu Shija amsaidie huku akipiga
kelele za kuomba msaada.
Mtendaji
huyo alisema wakati mwanaume huyo akitoa msaada kwa mpenzi wake, ndipo
fisi alimng’ata usoni na ndipo aliposhindwa kutoa msaada na fisi huyo
aliendelea kumshambulia mwanamke huyo hadi alipopoteza maisha papo hapo.
Kwa
mujibu wa mtendaji huyo, muda mfupi wananchi walifika eneo hilo wakiwa
na baadhi ya askari wa kituo kidogo cha polisi Ziba kisha kufanikiwa
kumuua fisi huyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Willibrod
Mutafungwa, alithibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo kwa kushambuliwa na
fisi na kwamba fisi huyo aliuawa.
Kwa
mujibu wa Kamanda Mutafungwa, majeruhi alikimbizwa Hospitali ya Rufani
ya Nkinga ambako alilazwa na kutoa wito kwa wananchi mkoani Tabora kuwa
makini na wanyama hatari kwa kutotembea usiku kwenye maeneo hatarishi
kwa ajili ya usalama wao.
0 comments:
Post a Comment