Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amewataka Watanzania kutumia
takwimu za sensa mbalimbali zinazotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu
ili kuongeza tija na hatimaye kupunguza umasikini nchini.
Mhe.
Mpina ametoa wito huo jana Jijini Dodoma, alipokuwa akizindua matokeo
ya utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016/2017 ukiwa ni utafiti wa pili
kufanyika nchini ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2014/2015.
“Tunapenda
kufanya sensa lakini mwisho wa siku hakuna anayetumia sensa hiyo.
Huwezi kufanya mapinduzi ya kiuchumi bila ya kutumia matokeo mbalimbali
ya tafiti,” alisema Mhe. Mpina.
Aliendelea
kusema, matokeo ya tafiti hizo yametumika katika kupima mchango wa
shughuli za kilimo katika Pato la Taifa, ambapo takwimu zinaonesha kuwa
mwaka 2014 uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.10 wakati mwaka 2017 uchumi
ulikuwa kwa asilimia 7.1. Aidha mchango wa shughuli za kilimo kwa mwaka
2014 ulikuwa asilimia 28.8 wakati mwaka 2017 ulikuwa asilimia 30.1.
Vile
vile amesema, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa zao la mahindi mwaka
2016/2017 uzalishaji wake ulikuwa tani 5,766,984 na kwa takwimu za
utawala za mwaka 2017/2018uzalishaji ni tani 6,681,000. Katika mwaka
2017 ongezeko la thamani ya shughuli za kilimo cha mazao iliongezeka na
kufikia shilingi trilioni 5.3 kutoka shilingi trilioni 5.1 mwaka 2016.
Mhe.
Mpina amesema, kwa upande wa Tanzania Baramkoa wa Mbeya umeendelea
kuongoza katika uzalishaji wa zao la mahindi kwa tani 578,280 (10%)
wakati Mkoa wa Morogoro umeongoza.
Aidha
kwa upande wa mifugo, Tanzania Bara inaidadi ya ng’ombe 30,496,687,
mbuzi 18,947,657, kondoo 5,565,468 na kuku wa asili 38,595,106 ambapo
mikoa inayoongoza kwa asilimia kubwa ya ng’ombe ni pamoja na Tabora
(8.7%), Mwanza (7.9%) na Manyara (7.2%).
Tanzania
Zanzibar ina idadi ya ng’ombe wapatao 175,314, mbuzi 107,993, kondoo
517 na kuku wa asili 1,754,786 na mikoa inayoongoza kwa asilimia kubwa
ya ng’ombe kwa Tanzania Zanzibar ni Kaskazini Pemba (30.3%) ikifuatiwa
na Kusini Pemba (19.9%).
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina
Chuwa amewaomba watumiaji wa takwimu hizo kuzitumia kwa manufaa ya
kufuatilia na kutathimini mipango ya maendeleo ya sekta ya kilimo,
mifugo na uvuvi na si vinginevyo.
Hata
hivyo amesema, Tanzania bado ni nchi ya pili katika Bara la Afrika kwa
kuwa na mifugo mingi hivyo ni dhahiri kuwa uwezo wa viwanda vya nyama
hapa nchini na kuuza nyama na bidhaa zake zinazozalishwa kwa lengo la
kujipatia fedha za kigeni.
0 comments:
Post a Comment