Spika
wa Bunge Job Ndugai ameitaka Serikali kuhakiki mikataba yake na
wawekezaji badala ya kusubiri kuwaadhibu wanaohusika na mikataba mibovu.
Akifungua
semina ya Chama cha Wabunge walio katika mapambano dhidi ya rushwa
(APNAC) bungeni jana Mei 21, Ndugai alisema wabunge wanafahamu namna
ambavyo mikataba ilivyoigharimu nchi.
“Eneo
hili la mikataba hasa kwa kampuni za nje ya nchi katika madini, nishati
za gesi, umeme imekuwa mibovu sana. Tumeliwa sana katika mikataba
hii,” alisema.
Alitaka eneo hilo kuangaliwa kwa umakini ili kuwa na mikataba safi.
“Lazima
tuhakikishe tumeziba mianya yote. Sasa hivi inaaminika kuwa rushwa
imepungua sana, japo kuna wengine wanasema imebadili sura na imekuwa
rushwa kubwa zaidi ya zile za zamani. Sasa hatujui lipi ni kweli inabidi
tulifanyie kazi.
“Tusije
tukaenda likizo tukidhani imepungua ama imeisha kumbe bado iko huko
iliko. Bunge linapambana sana na masuala ya rushwa kupitia kamati zote
za Bunge lakini zinazoshika bendera ni zile za usimamizi,” alisema.
Awali
akimkaribisha Spika Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika alisema inaonyesha
kuwa rushwa inapungua nchini.
0 comments:
Post a Comment