Mbunge
wa Arumeru Mashariki (Chadema) Joshua Nassari amesema Serikali
imewarudisha Watanzania katika kipindi cha ukoloni ambako waliporwa
ardhi yao bila sababu za msingi.
Nasari
amesema kitendo cha kuwachomea nyumba wananchi wa Meru kinawakumbusha
miaka ya 1950, ambapo walilazimika kuchanga fedha na kumtuma Japhet
Kilila Nguro kwenda Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutetea ardhi yao.
Akichangia
katika hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii, jana Mei 21, mbunge
huyo alizungumza kwa hisia kali kuwa jambo kama hilo linawakumbusha
mbali Watanzania na kuona kuwa bado wako katika kipindi cha ukoloni
walipokuwa wakiporwa ardhi bila hata kusikilizwa.
“Mimi
sijui tunawasaidia akina nani Tanzania yetu hii, wafanyabiashara
wanalia, wavuvi wanalia, wananchi wanalia na mnawapora ardhi hivi
mnataka kutawala nani lakini?” Alihoji Nasari
Alisema
mali walizoachiwa Watanzania na Mungu zimeshindwa kuwa baraka tena na
badala yake zimegeuka kuwa laana kwa Watanzania na kuwafarakanisha.
“Mnatutonesha
kidonda sisi watu wa Meru, angalia picha hizi zinaonyesha haya ni
maganda ya risasi na hizi ni picha za mifugo ambayo imedhoofu sana
iliyosababisha wananchi kubaki maskini kabisa,” alisema Nasari
0 comments:
Post a Comment