Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi,
amesema amewahi kushawishiwa na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
ili aweze kuhamia chama hicho tawala.
Ole Sosopi amesema hayo leo Mei 16 akiwa studio za EATV katika kipindi
cha KIKAANGONI kinachorushwa kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00
mchana hadi saa 10:00 za jioni na kuongeza kuwa yeye hana thamani ambayo
itaweza kumnunua kwakuwa ni tegemeo la vijana wa CHADEMA nchi nzima.
“Ndiyo nimewahi kushawishiwa na kiukweli ukiwa bora watataka kukuonesha
kwamba utakua bora zaidi, kumbe sio sahihi, ubora wa Ole Sosopi
unaoonekana leo CHADEMA, kama ningekuwepo CCM inawezekana ninsingepata
hata ubalozi wa nyumba kumi, naamini kule hawathamini uwezo bali ni nani
anakujua na historia yako” amesema Ole Sosopi.
Kiongozi huyo wa BAVICHA Taifa ameongeza kuwa watu hao walikua
wakimshawishi kwa kutumia njia ya kiurafiki kwa kumwambia kuwa kutokana
na ubora wake alistahili awepo upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Novemba 21, 2017 aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema
(BAVICHA) Patrobasi Katambi alitangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwa madai ya kufurahishwa na utendaji kazi wa mwenyekiti wa chama hicho
Rais Dkt. John Magufuli
Thursday, May 17, 2018
Nimeshawishiwa Kuhamia CCM- Mwenyekiti wa BAVICHA
Related Posts:
Jeshi la Magereza Lamjibu Sugu Jeshi la Magereza nchini limekanusha taarifa zilizoibuliwa na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kuhusu kukosekana kwa sare za wafungwa zaidi ya 600, katika gereza la Ruanda alipokuwa amefungwa. Msemaji wa Jeshi hilo L… Read More
Zitto Ahoji Uhalali Wa Mkuchika Kukaimu Uwaziri Mkuu Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amehoji ni kwanini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, George Mkuchika akaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni wakati kanuni za bunge haziruhusu. Amesema kwa mujibu wa kanuni za … Read More
CHADEMA yafukuza Wanachama Kwa Usaliti Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama. Waliofutwa uanachama ni pamoja… Read More
Ndugai aitaka Serikali kuhakiki mikataba yake na wawekezaji Spika wa Bunge Job Ndugai ameitaka Serikali kuhakiki mikataba yake na wawekezaji badala ya kusubiri kuwaadhibu wanaohusika na mikataba mibovu. Akifungua semina ya Chama cha Wabunge walio katika mapambano dhidi ya rus… Read More
Joshua Nassari: Serikali Inawarudisha Watanzania Enzi za Ukoloni Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema) Joshua Nassari amesema Serikali imewarudisha Watanzania katika kipindi cha ukoloni ambako waliporwa ardhi yao bila sababu za msingi. Nasari amesema kitendo cha kuwachomea nyumba… Read More
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment