Wabunge wameitaka Serikali kuviondoa vyama vya ushirika na kuruhusu uuzwaji wa mahindi nje ya nchi.
Hayo wameyasema jana jioni Mei 16, 2018 wakati wakichangia bajeti ya wizara ya kilimo ya mwaka 2018/19 bungeni jijini Dodoma.
Mbunge
wa Magu (CCM), Kiswaga Destery alisema, “kuna tatizo, wananchi
wanalalamika, wabunge wanalalamika, wananchi wamebaini wanaowapeleka
katika ushirika ni sisi wabunge na viongozi.”
“Suala
la ushirika wabunge wamelalamika wasikilizeni. Viongozi wa ushirika na
wahasibu wametumia rushwa kupita, wanakwenda kuwaibia wakulima na
wanunuzi wa pamba, mikataba tuliyonayo ni ya kukopa,” aliongeza.
Alisema,
“viongozi wamechaguliwa na watu saba au kumi, bora wangechaguliwa na
wananchi, mtawapa shida ma DC (wakuu wa wilaya), wakuu wa mikoa, hakuna
kazi watakayokuwa wanaifanya zaidi ya kulinda wezi.”
Kuhusu
zuio la mahindi, Destery alisema, “wabunge wanalalamika mahindi hapa,
bila kuweka utaratibu yataoza, ni vizuri serikali ikafungua na mahindi
haya yakiuzwa ndio mchango wenyewe na ndio maendeleo.”
Mbunge
wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga alisema, “inasikitisha sana kuona
kilimo kinaachwa kiholela holela, unaanzaje kumzuia mtu asiuze nje,
ninyi vipi mlitugea ninyi mtaji.”
Alisema wanapolima na kupata fedha “ndipo tunakwenda kuchangia huduma za jamii, sasa tunawezaje kujenga kama hatuna fedha.”
Kiwanga
alisema, “huu ushirika ni kama janga la taifa, Serikali imechukua hatua
gani kwa wale viongozi walioharibu ushirika, kama hamjachukua hatua
mtawafunga wengi na mtagombana na wengi sana.”
Alisema
bajeti ya kilimo iongezeke, masoko yawe wazi, mkulima aweze kuuza
kokote na kama mnataka kudhibiti wekeni mazao yenu lakini si kwa fedha
zake.
Mbunge
wa Urambo (CCM), Margaret Sitta alihoji kama wizara ya kilimo ina
kalenda ya misimu ya kilimo kwa kila mkoa kwani imezoeleka mbolea
kuwafikia wakulima kipindi cha kupalilia.
“Katika
mazao yenye matatizo ni tumbaku, tumbaku inaiingizia nchi hii zaidi ya
asilimia 40 ya fedha za kigeni. Hii changamoto tumekuwa tunazungumza
kila tunapopata nafasi, tatizo ni nini,” alihoji Sitta
0 comments:
Post a Comment