Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye
amesema kinachochangia kufa na kufungwa kwa biashara nchini kunatokana
na mazingira magumu ya biashara pamoja na sera kandamizi zilizopo.
Amesema
utafiti uliofanywa na TPSF umebaini kuwa biashara 4,640 zimefungwa
nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na vikwazo mbalimbali, huku
akibainisha kuwa mfuko huo kwa sasa upo tayari kusaidia maeneo
mbalimbali ya ujasiliamali pamoja na kutoa elimu.
Simbeye
ametoa kauli hiyo jana Mei 17, 2018 katika kongamano la kambi ya
ujasiriamali iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
Alisema
Tanzania inatakiwa kupiga hatua zaidi katika suala ujasiriamali kwa
sababu ni sekta pekee inayozalisha ajira kwa wingi nchini, hivyo ni
vyema ikatumika kitaaluma katika kuwaandaa wanafunzi kufùndishwa kwa
vitendo wanapokuwa vyuoni.
“Sekta
binafsi ni mwajiri pekee wa kudumu katika maisha ya mtu ama watu hivyo
vijana wetu wanatakiwa kuwa wathubutu na kuondokana na uwoga kwani ni
tatizo kubwa kwa vijana wetu,”amlisema Simbeye.
0 comments:
Post a Comment